HOTUBA YA UFUNGUZI YA WAZIRI WA KATIKA NA SHERIA MHE. PROF. PALAMAGAMBA KABUDI (MB) KWENYE KIKAO KATI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA MTANDAO WA WA WATETEZI WA HAKI ZA BINDADAMU NCHINI TANZANIA (TANZANIA HUMAN RIGHTS DEFENDERS COALITION- THRDC) TAREHE 3 JUNI, 2021 KWENYE UKUMBI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MTUMBA

1. Mhe. Geophrey Pinda – Naibu Waziri wa Katiba na Sheria;
2. Prof. Sifuni E. Mchome -Katibu Mkuu;
3. Bw. Amon A. Mpanju – Naibu Katibu Mkuu;
4. Wakurugenzi wa Wizara ya Katiba na Sheria;
5. Michael Kyande – Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania;
6. Bw. Onesmo Olengurumwa – Mratibu wa Mtandao wa Shirika la Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania;
Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu;
7. Bw. William Mtwazi – Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu;
8. Bi. Fatma Toufiq – Shirika la Women Wake Up;
9. Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania
(Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA);
10.Mwakilishi wa Shirika la Haki Elimu;
1

11.Mwakilishi wa Shirika la Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organisation;
12.Mwakilishi wa Shirika la Wote Sawa;
13.Mwakilishi wa Shirika la Door of Hope Tanzania; 14.Mwakilishi wa Shirika la Tanzania Peace Legal Aid; 15.Mwakilishi wa Shirika la Msichana Initiative; 16.Mwakilishi wa Shirika la The Pastoralists Indigenouos
Non- Governmental Organisations (PINGOs FORUM); 17.Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara ya Katiba na
Sheria;
Waandishi wa Habari;
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wageni wetu kutoka Shirika la Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bindadamu nchini Tanzania. Karibuni Mtumba, Karibuni Mji wa Serikali na Karibuni sana Wizara ya Katiba na Sheria.
Awali ya yote napenda kuwapongeza kwa uamuzi wenu wa kutaka kukutana na Wizara ya Katiba na Sheria kwa madhumuni ya kuzungumza na kujadili kuhusu maeneo ambayo tunaweza kushirikiana kutokana na majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria. Sisi kwa upande wetu tumeona umuhimu na faida ya kukutana na nyie ambao ni wadau wetu wakubwa kwa kuelewa
2

na kutambua kwamba shughuli zenu zinaendana na majukumu yetu ambapo walengwa na wanufaika ni watanzania. Masuala haya ya upatikanaji haki na haki za binadamu ni kati ya majukumu yetu makuu.
Mabibi na Mabwana;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 imeainisha Haki za Binadamu na Wajibu muhimu katika Sura ya kwanza, Sehemu ya tatu. Katiba pia inaitaka Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa na kuhakikisha sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa.
Aidha, wakati tunafurahia haki zetu za msingi lazima tukumbuke na tuelewe kwamba Katiba hii pia imeweka mipaka kwa haki na uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu. Ibara ya 30 ya Katiba inaeleza kwamba “Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma”
3

Hivyo kumekuwa na changamoto ya watu kusoma au kutafsiri Ibara moja ya Katiba bila kuzingatia Ibara nyingine na kutoelewa kwamba Katiba inasomwa kwa ujumla wake na siyo kunyambua ibara moja na kuitafsiri peke yake.
Vilevile kuna Changamoto ya kutoelewa kwamba Ibara za Katiba zinasomwa au kutafsiriwa kwa kuzingatia maamuzi ya Mahakama ambayo ndiyo mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki. Mahakama imekuwa ikitimiza vizuri jukumu lake la utoaji haki kwa kutoa tafasiri ya masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu mashauri ya Haki za Binadamu. Mahakama imekuwa ikitafasiri haki za binadamu kwa kutumia kanuni mbalimbali na kwa kuzingatia muktadha wa mazingira na nyakati. Aidha, Mahakama zetu zimekuwa zikitoa maamuzi stahiki kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu ambayo ni usawa na kutobagliwa.
Kuhusu kuwepo na mipaka kwenye haki za binadamu, kwenye shauri la Julius Ishengoma Francis Ndyanabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CIVIL APPEAL NO. 64 OF 2001, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilieleza kwamba hakuna uhuru usio na mipaka na Mahakama ilieleza kama ifuatavyo-
“Fundamental rights are not illimitable. To treat them as being absolute is to invite anarchy in society”
4

Mahamaka pia imetoa maamuzi kwenye masuala ya kutobaguliwa na haki za wanawake. Katika shauri la Holaria Pastory and Another(High Court of Tanzania at Mwanza (PC) Civil Appeal No. 70 of 1989. Reported in [1990] LRC (Const) 757). Mahakama Kuu ilieleza kwamba enzi za ubaguzi wa kijinsia zimeshapitwa na wakati kwani binadamu wote ni sawa. Mahakama hiyo ilieleza kama ifuatavyo;-
However the Senior District Magistrate of Muleba Mr. L.S. Ngonyani did not think the courts were helpless or impotent to help women. He took a different stand in favour of women.
He inter alia, said in his judgment:
What I can say here is that the respondents claim is to bar female clan members on clan holdings in respect of inheritance and sale. That female clan members are only to benefit or enjoy the fruits from the clan holdings only. I may say that this was the old proposition. With the Bill of Rights of 1987 (sic) female clan members have same rights as male clan member.
5

And as long ago as in 1968 Mr. Justice Saidi (as he then was) pointed out the inherent wrong in this discriminatory customary law. It was in the case of Ndewawiosia d/o Mbeamtzo v. Imanuel s/o Malasi (supra). He inter alia, said:
Now it is abundantly clear that this custom, which bars daughters from inheriting clan land and sometimes their own father’s estate, has left a loophole for undeserving clansmen to flourish within the tribe. Lazy clan members anxiously await the death of their prosperous clansman who happens to have no male issue and as soon as death occurs they immediately grab the estate and mercilessly mess up things in the dead man’s household, putting the widow and daughters into terrible confusion, fear, and misery. It is quite clear that this traditional custom has outlived its usefulness. The age of discrimination based on sex is long gone and the world is now in the stage of full equality of all human beings irrespective of their sex, creed, race or colour.
Mahakama pia imekuwa ikiangalia nguvu za mamlaka za utoaji haki na mwenendo kwenye mfumo mzima wa utoaji haki. Kwenye
6

kesi ya Dickson Paulo Sanga dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Miscelenoeus Civil Cause No. 29 ya 2019. Muombaji alikuwa anakipinga kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20 kwamba kinakiuka ibara za 13(3) na (6) na 15(1) na (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mahakama Kuu ilishawishika na kukifuta Kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania) ambacho kilikuwa kinaweka utaratibu kuhusu masuala ya dhamana katika kesi kubwa ikiwemo mauaji, uhaini, ugaidi, uhujumu uchumi, ubakaji na nyingine za aina hiyo. Ilibidi suala hilo lifikishwe na Serikali katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupitia kesi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi Dickson Paulo Sanga katika Civil Appeal No. 175 ya 2020 ambapo, hatimaye, mahakama hiyo ilirekebisha sintofahamu iliyokuwa inajitokeza baada ya kujiridhisha kuwa kifungu hicho hakikuwa kinavunja Katiba katika masuala ya Haki za binadamu.
Kwenye shauri la Jeremiah Mtobesya vs Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Misc, Civil Cause No, 29 of 2015 Muombaji alikuwa anakipinga kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20 kwamba kinakiuka ibara za 13 (6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo
7

Mahakama Kuu ilishawishika na kukifuta Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania) ambacho kilikuwa kinampa Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana Mahakamani. Mahakama ya Rufaa ilibatilisha kifungu hicho cha 148(4) kwamba kinakiuka ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika kesi ya Jebra Kambole dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Miscelenoeus Civil Cause No. 22 ya 2018, Kambole alikuwa anapinga kifungu cha 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kwamba kinakiuka ibara za 12 (2), 13(1 )(2)(6)(a), (d)(e), 14 and 29(1 )&(2) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mahakama kuu ya Tanzania iliyatupilia mbali Maombi hayo na ilieleza kwamba suala hilo tayari lilishamuliwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwenye kesi ya Mbushuu alias Dominic Mnyaroje and another vs Republic [1995] TLR 97 ambapo ilisema adhabu ya kifo haikinzani na Katiba.
Mabibi na Mabwana,
Serikali pia imeweka mifumo ya kitaasisi ya kulinda na kukuza haki za binadamu na utawala bora. Ibara ya 129 ya Katiba ya
8

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 imeanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pia inatekeleza majukumu yaliyokuwa ya “The Permanent Commission for Enquiry (PCE)” iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 67 na 68 ya Katiba ya Mapitio ya Mwaka 1965 “Interim Consititution” Shughuli za PCE zilikuwa kuchunguza ukiukwaji wa utawala “mal-administration”
Kutokana na historia hiyo Tume ina kazi kubwa mbili; Taasisi ya Taifa ya Haki za Binadamu “National Human Rights Institution” pamoja na Chombo cha Uchunguzi “Ombudsman.” Hivyo kuitwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni sahihi kabisa. Masuala ya Haki za Binadamu yanatekelezwa kutokana na Tume kuwa Taasisi ya Taifa ya Haki za Binadamu na inatekeleza masuala ya Utawala Bora kutokana na Tume kuendeleza shughuli za PCE.
Tume ilianza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2001 baada ya kutungwa kwa Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya 2001 na GN Na. 311 ya tarehe 8 Juni 2001. Sheria hi imeainisha majukumu ya Tume ambayo ni pamoja na:
a) Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi;
9

b) Kupokea malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu kwa ujumla;
c) Kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
d) Kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
f) Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo vifungu vya sehemu hii vinahusiana katika utaratibu wa kawaida wa kutekeleza kazi za ofisi yake au utendaji wa kazi unaokiuka mamlaka yake;
g) Kuchunguza malalamiko yanayohusiana na utekelezaji au utendaji wa watu wanaoshikilia ofisi katika utumishi wa Serikali, mamlaka za umma au vyombo vya umma, ikijumuisha taasisi binafsi na watu binafsi ambapo malalamiko hayo yanadaiwa kuwa ni ya matumizi mabaya ya madaraka, huduma za upendeleo kwa mtu yeyote, ikiwa ni mlalamikaji au mtu mwingine, katika kutekeleza kazi zao za kiserikali au umma;
Serikali pia inatambua kwama mfumo bora wa sheria ndiyo msingi wa kutekeleza matakwa ya Katiba, sera na mipango ya nchi. Hivyo, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ilianzishwa
10

kupitia Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Sura ya 171 ya Sheria za Tanzania). Maboresho ya sheria hufanyika kwa lengo la kuendeleza na kuboresha sheria ili ziende na wakati na kwa namna endelevu. Katika kipindi cha 2015-2020 Tume ya Kurekebisha Sheria ilikamilisha utafiti na mapitio ya mifumo ya sheria 11 zikiwemo; Mfumo wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (Sura ya 410 ya Sheria za Tanzania), Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Huduma kwa Wazee; Mfumo wa sheria kuhusu haki za walaji na watumiaji wa bidhaa; Mfumo wa Sheria zinazohusu masuala ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu; Mfumo wa Sheria zinazosimamia Haki Jinai na Mapitio ya Sheria ya Ushahidi na Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazohusiana na Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi.
Tume ya Taifa ya Kurekebisha Sheria ina majukumu maalum ya kuhakikisha sheria zetu zimezingatia matakwa ya Katiba. Hivyo, tunawasihi sana kutumia chombo hiki na endapo mnakutana na changamoto mbalimbali kwenye sheria zetu muwasilishe hoja zenu kwenye chombo hiki ili kifanye uchambuzi na kutoa mapendekezo kwa Serikali.
Mabibi na Mabwana;
11

Kwa kutambua changamoto ya wananchi kwenye suala la upatikanaji haki Sheria ya Msaada wa Huduma za Sheria, Sura ya 21 ilipitishwa mwaka 2017. Sheria hii imekuwa ikitekelezwa chini ya uratibu wa Wizara ya Katiba na Sheri na hadi sasa kuna mafanikio yafuatayo:
i. Msajiliameteuliwa
ii.Wasajili wameteuliwa kutoka kila Mkoa, Wilaya na
Halmashauri zote nchini na jumla yao wapo 209.
iii.Mfumo wa Kielektroniki wa usajili na kutoa taarifa umeandaliwa na unafanya kazi. Tayari umesajili Watoa
Huduma 158 na Wasaidizi wa Kisheria 620
iv. Ukaguzi wa Watoa Huduma umefanywa katika mikoa yote 26.
v. Elimu juu ya Sheria hii inaendelea kutolewa kupitia Wiki ya Msaada inayofanyika kila mwaka nchini pamoja na maadhimisho mbalimbali ya kitaifa.
Mabibi na Mabwana;
Serikali kwa kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imekuwa ikishiriki kwenye mikutano ya Kimataifa na Kikanda ya Haki za Binadamu na Haki za Watu kama Baraza la Umoja wa Matiafa la Haki za Binadamu na Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa ngazi ya Vikao vya Mawaziri na vikao vya wataalam. Hii ni kwa sababu Serikali inatambua na inaheshimu wajibu wake kama
12

mwanachama wa vyombo vinavyosimamia jitihada za nchi za kukuza na kulinda haki za binadamu na haki za watu.
Serikali pia imekuwa ikishiriki kwenye Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mapitio Katika Kipindi Maalum kila baada ya miaka minne bila kukosa. Vilevile tunawapongeza sana Asasi zisizo za Kiserikali kwa kushiriki kwenye mfumo huu na kuwasilisha taarifa yenu ndani ya muda. Tunapenda kuwapongeza kwa kushiriki kwenu kikamilifu kwenye mfumo wa umoja wa mataifa wa mapitio katika kipindi maalum (UPR). Katika huu mzunguko wa tatu tumeona namna ambavyo mmejipanga kwa kushirikiana na asasi nyingine zisizo za serikali na mmeweza kuwasilisha taarifa yenu chini ya mfumo huu. Aidha, tunawapongeza sana kwa namna ambavyo mmekuwa mnaishirikisha Serikali kwenye vikao vyenu ambayo kimsingi ndiyyo vinavyongoza mfumo huu. Hongereni kwa kuweza kuwasilisha taarifa yenu na tutaendelea kuboresha utekelezaji wa mfumo huu pamoja na kuimarisha ushirikiano wetu wakati wa kutekeleza mfumo huu pamoja na mifumo mengine ya kikanda na kitaifa ya haki za binadamu na haki za watu.
Mabibi na Mabwana;
Nyie kama watetezi wa haki za binadamu mna jukumu na uwezo mkubwa siyo tu katika kuwatetea watu lakini pia katika kulinda na
13

kukuza haki za binadamu na haki za watu pamoja na masuala ya utawala bora na utii wa sheria. Hivyo, tuko tayari kushirikiana na nanyi pamoja na wadau wengine wote wasio wa Serikali ambao wako tayari kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza na kulinda haki za binadamu na watu.
Asasi zisizo za Serikali zina nafasi na wajibu mkubwa katika kukuza na kulinda haki za binadamu na haki za watu pamoja na kuleta maendeleo nchini. Hivyo, lazima tuwapongeze katika juhudi hizi kwa mfano kuna mafunzo ya Majaji yanayoendelea ambayo taasisi yenu imeratibu. Pia mmeonyesha nia ya kuanza kutekeleza maeneo yenu kwenye Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo na hatimaye kuunga jitihada za Serikali za kukuza na kulinda haki za kisiasa, kiraia, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
Asasi zisizo za Serikali zinashiriki katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu ya Dunia ambapo Wizara yangu inasimamia utekelezaji wa Lengo la 16 linalohusu amani, haki na mashirika imara “peace, justice and strong institutions.” Serikali iliwasilisha taarifa yake ya hiari ya utekelezaji ya Malengo Na 4.,8,10,13,16 na 17 Julai 2019 kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa. Taarifa hiyo inaonyesha namna ambavyo Asasi zisizo za Serikali zinachangia kutekeleza malengo hayo yanayohusu elimu, kazi na
14

maendeleo ya kiuchumi, usawa, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, na masuala ya ushirikiano.
Vilevile mna nafasi katika utekelezaji wa Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika. Tanzania ilishiriki kwenye tathmini ya utekelezaji wa Agenda Na. 1,2,3,4,5,6,7 zinazohusu maisha bora, elimu, afya, maendeleo ya kiuchumi, kilimo ya kisasa, uchumi wa bahari, na mazingira. Aidha, ni matarajio yetu kwamba ushirikiano na nyinyi utaendelea ili tuweze kutoa taarifa stahiki wakati tukitoa taarifa ya utekelezaji wa Agenda Na. 11 inayohusu msingi wa demokrasia, haki za binadamu, haki na utawala wa sheria.
Mabibi na Mabwana;
Napenda kufafanua kwamba haya yote pia ni matakwa ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025. Serikali imeahidi kuheshimu na kuzingatia mifumo ya kulinda haki za binadamu, kwa mtu mmoja mmoja, makundi na jamii kwa ujumla (118.b); Kubuni na kutekeleza mikakati ya kukuza, kulinda na kutekeleza misingi ya haki za binadamu na wajibu wao (118.c); Kuweka mazingira rafiki kwa wananchi kufikia vyombo vinavyosimamia haki katika ngazi zote (118.d); Kulinda haki za kikatiba za wananchi wanaoshiriki katika mijadala mbalimbali inayohusu maendeleo ya Taifa lao na kutoa elimu kwa umma juu ya
15

masuala ya katiba na sheria ili kuimarisha misingi ya kikatiba (constitutionalism), demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria (120.a); Kuchukua hatua zaidi za kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani(120.b); Kuimarisha mfumo wa wasajili wasaidizi katika halmashauri zote ili kuwezesha uratibu na utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi, ikiwemo msaada wa huduma za kisheria kwa masuala ya mirathi na ndoa(120.c); Kuhakikisha huduma bora za sheria zinapatikana kwa wakati na kwa gharama nafuu kwa kuongeza wataalam, miundombinu, vitendea kazi na kusogeza huduma karibu na wananchi (120.d); Kuimarisha vyombo vya sheria kwa kuongeza wigo wa huduma za utoaji wa haki nchini(120.e).
Hivyo, tuko tayari kushirikiana na nyinyi wadau wetu kwenye masuala ya upatikanaji haki na masuala ya haki za binadamu. Tunaelewa kwamba mtakuwa na vipaumbele vyenu na Serikali pia ina vipaumbele vyake ambayo vinalenga kukuza na kulinda haki za binadamu na watu na kuwaletea watanzania na nchi yetu maendeleo. Hayo hapo juu ni maeneo ambayo tuko tayari kushirikiana na nyinyi bega kwa bega na hatua kwa hatua kwa kuwa tuna lengo moja, kuimarisha maisha ya watanzania, kuwaletea maendeleo na kudumisha amani.
16

Baada ya haya maneno machache nawakaribisha tena Wizara ya Katiba na Sheria.
ASANTENI SANA.

Author

MontJali